Shafii Kassim Mpenda
Chama cha akiba na mikopo cha Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN) TSN Saccos leo kimefanya uchaguzi wake mkuu wa nafasi mbalimbali ikiwemo ya uenyekiti na wanachama kumchagua Shafii Mpenda kuwa Mwenyekiti Mpya wa Saccos hiyo.
Mpenda amechaguliwa kushika nafasi iliyoacha wazi kufuatia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa awali Dasu Steven aliyehamishiwa Mkoani Mwanza kikazi.
Wakati Mpenda kutoka Idara ya Uhasibu akipata kura 50 dhidi ya mpinzani wake Mgaya Kingoba wa Idara ya Habari alipata kura 26, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ikienda kwa Peter Francis nae kutoka Uhasibu aliyembwaga Mkuu wa Kitengo cha Matangazo Felix Mushi ambaye alishindwa kutetea nafasi yake.
Aidha wanachama wengine waliojitokeza kuwania nafasi hizo ni pamoja na Faraja Mgwabati, Kanaeli Kaale, huku uchaguzi huo ukisimamiwa na maofisa Ushirika toka Ushirika Makao Makuu.
Hongera sana Shafi, mie nakukubali sana, wana TSN wamechagua vyema kabisa! Najua kwa uwepo wako kwenye hiyo nafasi lazima tuone maendeleo makubwa na usawa utakuwepo. Kila lakheri mkuu, unastahili pongezi. Mungu akubariki sana katika kipindi chako cha uongozi.
ReplyDelete