Ikiwa Tanzania inasherehekea miaka 50 ya UHURU, mbunifu wa kiafrika Mustafa Hassanali’s, atazindua “UHURU” collection ambayo alivutiwa na muonekano wa bendera ya taifa kama iliyopeperushwa Mt Kilimanjaro tarehe 9 Desember 1961 AFI Afrika Fashion Week iliyopo Johannesburg Afrika Kusini.
“Mkusanyiko huo wa mavazi umehusisha maliasili ya Tanzania, Ambao watu wake ni wenye ukaurimu , nchi yenye utajiri wa maliasili za taifa na pia ni nchi iliyojengeka na misingi aloiweka Baba wa taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere” alisema Mustafa Hassanali
Mkusanyiko huo wa mavazi umepewa jina la UHURU. Na pia haupo tu kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bali uhuru huo kuonyesha uwito, ubunifu na utamaduni.
Kwa kuwa taifa moja, Mkusanyiko huo wa mavazi utaonyesha Amani na utengenezaji wa mavazi hayo yataielezea Tanzania kiundani kupitia mbunifu wake kutoka Tanzania Mustafa Hassanali.
Safari ya Mustafa Hassanali ya Afrika kusini imedhaminiwa na Precision Air, Shirika la ndege lenye ukuaji mkubwa Tanzania ambalo kwa sasa linafanya misafara yake mara 5 kwa wiki kwa misafara ya Johannesburg.
“Tunafarijika kuwa na ushirika na Mustafa Hassanali, ambae atafanya maonyesho ya mkusanyiko wake wa mavazi kwa mara ya nane Afrika kusini. Muungano wetu mpya unaangalia kutangaza biashara,utalii na utamaduni uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. alisema Afisa uhusiano wa Precision air Annette Nkini.
Ikiwa ni mara ya kwanza tena kwa Mustafa Hassanali, Atakuwa ni mbunifu pekee ambae atasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzanian nje ya Tanzania kwa kufanya ufunguzi wa mkusanyiko wake wa Mavazi Afrika kusini.
“Maonyesho ya UHURU collection yatakuwa ni maonyesho yangu ya pili AFI Africa Fashion Week na ya nane kwa jamuhuri ya Afrika kusini, Itakayokuza mahusiano ya pande mbili kati ya Tanzania na Afrika Kusini.” Aliongeza Hassanali
AFI Africa Fashion week inamilikiwa na African Fashion Internationals Dr Precious Moloi, itakayofanyika Sandton Convention Centre kuanzia tarehe 20-22 October. Mustafa Hassanali ndo mbunifu pekee kutoka Tanzania aliealikwa katika wiki ya kujivunia na atafanya maonyesho yake tarehe 22 October saa 10 jioni
0 comments:
Post a Comment