KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BONGO 5 MEDIA ZAWAKUTANISHA WASANII WATAKAOTUMBUIZA KATIKA TAMASHA LA BIA TANZANIA
Dar es Salaam Septemba 29, 2011- Wasanii zaidi ya kumi watakaotumbuiza katika Tamasha la kwanza la Bia Tanzania Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam wameahidi kutoa burudani ya aina yake kwa watanzania.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wasanii hao na wawakilishi waliishukuru Bia ya Kilimanjaro Premium Lager na Kampuni ya Bongo 5 kwa kuandaa tamasha hili kubwa la kwanza na la aina yake Mkoani Dar es salaam, .
Baadhi ya wasanii na makundi yaliyohudhuria mkutano huo na waandishi wa habari ni Chidi Benz, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta, Akudo Impact, Canal top, Tip Top, Ben Paul, Linex, Linah na THT ambao waliwapa wandishi wa habari vionjo kidogo ya vitu ambavyo watavifanya katika tamasha hili.
Kilimanjaro Premium Lager ikishirikiana na Kampuni ya Bongo 5, Alliance Francaise na Taasisi ya Goethe wanandaa tamasha kubwa la bia la kwanza Tanzania ambalo litafanyika katika Viwanja vya Leaders Octoba 1 na 2 mwaka huu.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Bw. George Kavishe alisema tamasha hili litakalojulikana na Kilimanjaro Beer Festival, litakuwa la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Dar es salam, Mwaka 2007 tuliandaa tamasha kama hili Mkoani Kilimanjaro na 2008 tulifanya Mkoani Arusha na yalikuwa na mafanikio makubwa, sasa tunafanya Dar es salaam tukiwa na madhumuni ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na kuwaleta Watanzania pamoja.
Alisema miongoni mwa waalikwa ni wasanii mbalimbali wa Bongo Movies ambao watajichanganya na watu na kubadilishana mawazo nao na kucheza mechi ya kirafiki na timu zambalimbali za Veterani.
Tamasha hilo litaanza saa nne kamili asubuhi na litaendelea kwa siku mbili mfulululizo, hadi usiku na kwamba tiketi zitauzwa Tsh 10,000 kwa siku zote mbili na Tsh 7,000 kwa siku moja.
Bw. Kavishe aliwaasa Watanzania kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo ili waburudike na kujivunia mafanikio yao baada ya miaka 50 ya Uhuru.
Kwa upande wake, Mratibu wa Matukio, Olive Nimaga aliishukuru TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa jitihada zake za kuwatambua na kuwathamini wateja wake kwa kukukubali kudhamini tamasha hilo la aina yake.
Baadhi ya wanamuziki na waandaaji wa tamasha hilo wakiwa katika picha ya pamoja hhii leo |
“Tunawahakikishia mazingira mazuri na salama wakati wa tamasha hili kwani itakuwa wikiendi yenye burudani mbalimbali,” alisema.
Alisema baadhi ya wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Linah, Linex, Chidi Benz, Godzilla, Offside Trick, Akudo Impact, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wengineo. “Kutakuwa na nyamachoma na vyakula vingine vya aina mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment