Nafasi Ya Matangazo

September 27, 2011

Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.
  Mtoto Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.
   Cecilia amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.
   Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
   Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
   Mtoto huyu aliondoka hapa nchini jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja  na mlezi mmoja mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa  na madaktari tayari kwa uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
Posted by MROKI On Tuesday, September 27, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo