Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa mhadhara na kuelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden. Mhadhara huo uliambatana na safari ya Makamu wa Rais katika maabara mbalimbali zilizopo chuoni hapo jana Sept. 26, 2011.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Prof. Mohamed Hassan (kushoto) Prof. Jean-Piere Ezin (wapili kushoto) na Prof. Mohamed Elton, baada ya kumalizika kwa Mhadhara wa kuhusu changamoto za sayansi wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Idara ya Sayansi za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uppsala kilichopo Sweden, jana Septemba. 26.2011
0 comments:
Post a Comment