Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho kikwete,akifuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,walifika katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar kuona maiti mbali mbali zilizofariki katika tukio la ajali Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini ikielekea Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akishauriana jambo na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad,baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Hospitali ya Kivunge.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwafariji majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Askari wa vikosi nbali mbali vya ulinzi wakibeba majeruhi waliookolewa katika meli iliyozama huko katika Bahari ya Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja,wakifikishwa katika ufukwe wa Nungwi.
Askari wa vikosi vya ulinzi wakiwa katika doriankuhakikisha usalama unapatikana kwa raia wakati wa upokeaji wa majeruhi waliokolewa katika meli iliyozama ya Mv Spice Islander,ikitokea Unguja kuelekea Pemba.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akimfariji Ramadhan Haji,mkaazi wa Saateni Mjini Unguja, majeruhu wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein akiwafariji majeruhi wa ajali ya meli ya Mi Space Islander.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein, akiwafariji majeruhI wa tukio la kuzama kwa meli ya Mv Spice Islander,katika Ufukwe wa bahari ya Nungwi,mkoa wa Kaskazini Unguja.
huu kweli ni msiba mkubwa na ni pigo kubwa kiukwel! EE MUNGU ZILAZE ROHO ZA MAREHEM MAHALA PEMA PEPONI...AMEEEEN!!!!
ReplyDelete