Nafasi Ya Matangazo

September 22, 2011

 

Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi  cheti mmoja wa wahitimu  wa elimu ya  kidato  cha nne katika  shula ya Sekondari  ya  Doma iliyopo Wilayani humo , Mkoa wa Morogoro , ambaye pia anatarajia kufanya mtihani wake Oktoba mwaka huu , wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu  Shuleni hapo.
Mmoja wa watarajiwa wa kuhitimu masomo ya kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Doma, iliyopo Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, akiwa ameshikiria maboksi ya zawadi alizopewa na ndugu zake mara baada ya kutimitimshwa kwa  sherehe yamahafali ya pili ya kidato cha nne yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu  shuleni hapo, Mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla akikabidhi mipira mitatu kwa Mwanafunzi wa Kidato cha tatu , Husna Salum , ambaye ni Kiongozi wa Michezo katika  Shule ya Sekondari Doma iliyopo Wilayani humo, Mkoa wa Morogoro, wakati wa mahafali ya pili ya Kidato cha Nne ya Shule yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu  Shuleni hapo.
Wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Doma, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, wakiimba nyimbo za kuwaaga wanafunzi wenzao, walimu , wazazi pamoja na mgeni rami ,Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla ( hayupo pichani) wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu, Shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi  vitabu 400 vyenya thamani ya sh: milioni tatu vya  mitaala ya masomo mbalimbali ya Sekondari vikiwemo vya sayansi , Kiingereza , kiswahili ,  fasihi ya kiswahili na hesabu kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Doma iliyopo Wilayani Mvomero , Mkoa wa Morogoro , John Makarius , kwa ajili ya matumizi ya  wanafunzi na  kuondoa tatizo ya ukosefu wa vitabu,  wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu  Shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero Amos Makalla ( suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu watarajiwa wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Doma iliyopo Wilayani Mvomero  wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha nne yaliyofanyika Septemba 21, mwaka huu, Shuleni hapo, wakiwemo pamoja na baadhi ya walimu  na viongozi wa Serikali ya Kata ya Doma.
Posted by MROKI On Thursday, September 22, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo