Nafasi Ya Matangazo

August 18, 2011


Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2011 wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Tarangire mkoani Manyara jana walipjwenda kujionea wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo ya tano kwa ukubwa nchini. Warembo hao wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani kwa watanzania. Katika hatua nyingine leo Miss Photogenic anataraji kutangwazwa na kujipatia tiketi ya kuingia katika nusu fainali ya shindano la Vodacom Miss Tanzania. Miss Photogenic atakuwa ni mrembo wa pili kuingia katiak hatua hiyo ya 15 bora baada ya Top Model. 
 Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wanataraji leo kutembelea ofisi za Vodacom mjini Arusha zilizopo Ngarenaro katika jengo la Summit Tower. Wakiwa katika ofisi hizi mbali na kupata taarifa za shughuli mbalimbali pia watazungumza na waandishi wa habari na kutangazwa kwa mshindi wa Miss Photogenic 2011 ambaye atajipatia tiketi ya kuingia hatua ya Nusu fainali ya shindano hilo.
Posted by MROKI On Thursday, August 18, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo