Nafasi Ya Matangazo

August 18, 2011

Mchezaji wa timu ya Simba Patrick Mafisango akihojiwa na waandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Malimani Televisheni, mara baada ya kupokea zawadi yake ya shilingi laki tano kutoka kwa Benki ya NMB kutokana na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kati ya Yanga na Simba kwenye mchezo wa ngao ya hisani, ambao umemalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa na Simba kuibuka kidedea kwa kuifumga Yanga magoli 2-0. Mchezo huu pia umetumika kama uzinduzi rasmi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania inayotarajiwa kuanza mwezi huu katika viwanja mbalimbali nchini, Vodacom Tanzania ndiyo wadhamini wakuu wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 14 za Tanzaia bara.
Mchezaji wa Simba Uhuru Selemani akinyanyua juu ngao ya hisani mara baada ya kukabidhiwa rasmi katika mchezo wa ngao ya hisani, uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo usiku.
Katibu Mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Angetile Osiah akishangaa jambo mara baada ya mchezo wa ngao ya hisani kati ya Wekundu wa Msimbazi na Watoto wa Jangwani uliofanyika leo kumalizika, kulia ni George Rwehumbiza Mkuu wa udhamini wa Vodacom Tanzania na kushoto ni Makamu wa Kwanza wa TFF Athuman Nyamlani.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Kaburu Nyange akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo kulia ni Gervas Kago na Felix Sunzu.
Goli mbili zikonekana kwenye ubao wa matangazo.
Wachezaji wa Simba wakishangilia kutoka kulia ni Emmanuel Okwi, Victor Costa, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Juma K. Juma.
Mchezaji wa Simba Juma Nyoso akipeana mkono na Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza kulia ni katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah.
Hapa ni raha ya ushindi wakisakata mayenu kutoka kulia tena ni Victor Costa, Uhuru Selemani, Felix Sunzu na Juma K. Juma. 
Source: FULL SHANGWE BLOG
Posted by MROKI On Thursday, August 18, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo