Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta wa Idara ya Usimamizi na Uratibu wa Mifumo ya Teknolojia ya Habari wa Wizara ya Fedha Elimu sekeni (kulia) akitoa ufafanuzi jana kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha matukio yaliyopo katika vitabu vya picha katika maonyesho ya wakulima nane nane ya mjini Dodoma. Wageni hao ni Mfanyakazi kutoka Shirika la lisilokuwa la Kiserikali linalojulikana kama INADES Formation Tanzania Katja Flockau( kushoto) , Michael Mwenda( wa pili kushoto) na Christina Kamuga(wa pili kulia) wote ni wanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
Afisa fedha Mkuu (Principal Finance Officer) wa Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) Sostheness Mushema (wa pili kutoka kushoto) akimweleza mtumishi mstaafu wa umma kutoka Wizara ya Ujenzi Nassor Kijanga (kulia) juu hatua za kufuatilia katika kudai malipo yake ya uzeeni jana wakati mtumishi huyo alipotembelea katika banda la Wizara ya fedha kwenye maonyesho ya wakulima ya nane nane yanayoendelea mjini Dodoma. Wengine ni Mchambuzi wa Mifumo ya kompyuta wa Wizara hiyo Elimu Sekeni(wa pili kulia) na mwananchi aliyembelea maonyesho Joseph Nyamriba(kushoto)..
Mchumi kutoka Idara ya Bajeti ya Wizara ya Fedha Adam Msumule (kushoto) akitoa ufafanuzi jana kwa wageni waliotembelea banda la Wizara ya fedha kuhusu mgawanyo wa bajeti ya Serikali kuzingatia vipaumbele katika maonyesho ya wakulima nane nane ya mjini Dodoma wakati walipotembea banda la Wizara ya Fedha. Wageni hao ni Mfanyakazi kutoka Shirika la lisilokuwa la Kiserikali linalojulikana kama INADES Formation Tanzania Katja Flockau( katikati) , Michael Mwenda( kushoto) na Christina Kamuga( kulia) wote ni wanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma.
0 comments:
Post a Comment