Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2011

Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu za Mkononi wa Airtel  Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi T-shirt 100 kwa niaba ya Airtel  kusaidia shirikisho la Ngumi Tanzania, anaekabidhiwa ni Katibu wa chama  cha Waamuzi wa mchezo wa ngumi Taifa Juma Suleiman (katikati). T-shirt  hizo zitatumika   katika mashindano ya klabu bingwa ya Ngumi za Ridhaa  yanayoendelea sasa mkoani Mwanza kwa kushirikisha vilabu toka mikoa yote  na yatafikia kilele siku ya nanenane.wa kwanza kulia pichani ni Makoyo  Sangula Kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Ngumi


Akizungumza wakati wa makabidhiano yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam,  Katibu wa chama chama cha waamuzi wa michezo ya ngumi taifa, Juma  Suleiman alisema." Tunaishukuru kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa  kutupatia vifaa hivi vya mazoezi ambazo ni T-shirt zitakazotumika na  wachezaji wa vilabu shirika toka mikoa yote wakati wa mashindano.

Hii  inaonyesha kuwa mnadhamira ya dhati ya kusaidia na kuinua kiwango cha  mchezo wa ngumi nchini Mashindano haya ya club bingwa ya taifa  yanahusisha timu za mkoa na vilabu mbalimbali  hapa nchini kwa lengo la  kujiaandaa na mashindano ya kimataifa ya All African Game  yatakayofanyika msumbiji, hivyo basi tunapenda kuwakaribisha wakazi wote  wa jiji la Mwanza kuona mashindano haya  ni kivutio kikubwa  aliongeza  Bw Suleiman&nbsp

Akikabidhi msaada huo Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson  Mmbando alisema Airtel imejipanga katika kuchangia sekta ya michezo  nchini, Airtel tunaendelea na mkakati wetu wa kukuza michezo aina yote  nchini Tanzania na ndio maana leo hii tunaanza ushirika huu na wana  masumbwi Tayari tumejikita katiaka mashindano mpira wa miguu ya U-17 ya  Airtel rising star ambayo kwa sasa yamefikia ngazi ya nusu fainali, ni  matumani yetu kuwa ushirikiano mzuri kati yetu na wadau wa michezo kama  hawa watatuletea michanganuo endelevu ili tuendelee kuwa na wanamichezo  bora watakaoitangaza nchi yetu vyema katika mashindano mbali mbali.
Posted by MROKI On Wednesday, August 03, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo