Nafasi Ya Matangazo

August 15, 2011

AIRTEL FLAVA NDANI YA SHULE ZA SEKONDARI SANGARA YA CHANIKA-DIAMOND AFUNIKA

Airtel Tanzania imekua ikishiriki kikamilifu sana katika mchakato wa kukuza vipaji vya wanafunzi vikiwemo pia vipaji vya mpira wa miguu kupitia mradi maalum uliozinduliwa mwaka huu na mwanamichezo nyota wa kimataifa Andy Cole lengo ikiwa ni kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao katika vipaji walivyonanyo.  

Airtel imeendeleza hiyo pale Msanii wa kizazi kipya Dimond Platinumz alipoteka hisia za mashabiki wake wa shule ya sekondari  ya sangara  katika  shoo maarufu yenye lengo la kuvumbua vipaji  pamoja na kuelimisha wanafunzi iliyodhaminiwa na Airtel Tanzania  iliyofanyika mwishoni mwa wiki.             

Shoo hiyo ilitawaliwa na kelele za furaha pale msanii huyo mkali ajulikanaye kama  Rais wa wasafi alipopanda jukwaani akiwa ameambatana na wacheza shoo wake wanne.

Msanii huyo aliimba nyimbo zake mbalimbali zinazotamba zikiwemo Nenda kamwambie,Nitarejea, na Mbagala  uliompa umaarufu hapa nchini.

Diamond ambaye pia huwa sambamba na wacheza shoo wake katika kuonyesha umahiri wake aliweza pia kuwafurahisha wanafunzi waliokuwa wanamshangilia na vilevile kuwataka wanafunzi hao kuweka mkono mmoja juu kama ishara ya umoja.

Aidha waadhamini wa shoo hiyo Airtel walisema bado kampuni itaendelea na mtindo huo wakuwazawadia wanafunzi wa shule mbalimbali burudani ili kuwafanya wanafunzi waweze kupumzika baada ya kuwa kwenye masomo kwa muda mrefu

Bado airtel tutaendelea kushirikiana na waalimu na wanafunzi wa shule mbalimbali ili kuendeleza fleva za airtel wakiwa mashuleni, hii inawasaidia wanafunzi wafurahie na kuburudika  wakiwa masomoni. Hii ni kwa kuwa Airtel  tunaamini kuwa burudani ni sehemu ya elimu kwa wanafunzi” alisema Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Airtel pia iliwazawadia wanafunzi wa shule hiyo fulana,madaftarina pamoja na kofia.

Shoo hiyo ya Burudani na Flava za Airtel kwenye shule za sekondari hufanyika kila mwezi mara moja ambapo lengo lake ni kuibua vipaji mbalimbali vya sanaa kama kuimba ,kuonyesha mavazi na kucheza muziki  kwa wanafunzi wa shule za sekondari.
Posted by MROKI On Monday, August 15, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo