Hii ni Tanga, Ukiona vitu hivi utajua kuwa upo mkoani gani, maana kila mkoa unaminara ambayo inatambulisha mji husika. Huundio mnara mkuu wa Mashujaa wa Tanga.
Tanga bwana wanapenda sana kausafiri haka, na wake kwa waume wanakatumia.
Jengo la CCM Tanga
Tanga kuna club kazaa za muziki usiku, ipo hii, Chichi, Lacasa Chica na ingine yaitwa Pweza.
Huu pia ni moja ya mnara uliopo katika moja ya mizunguko ya Tanga
Na mwingine ni huu. Wenyejeji wanakwambia karibu Tanga...Tanga ya leo si kama ya zamani ambayo ukipiga kifuu wanadai kilikuwa kinasema na Si Waja leo waondoka leo na hasa ilikuwa ni kutokana na hivyo vituko. Lakini Tanga ya sasa Waja leo wakaa hapahapa na Raha jipe Mwenyewe Mwingine akikupa amekuongezea.




0 comments:
Post a Comment