Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akipata Maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Bw Nurdin Babu alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa kilwa Kuzinduwa Mradi wa Uhifadhi Misitu ya Ukanda wa Pwani iliyofanyika Jana
MADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
Watanzania wataungana na mataifa mengine Duniani kote kuadhimisha ya siku ya mazingira duniani
ambapo , Maadhimisho ya Siku hii kwa mwaka huu nchini, yatafanyika mjini Songea, mkoa wa Ruvuma
na yataambatana na uzinduzi wa sherehe ya kihistoria ya kumbukumbu za Taifa letu za maadhimisho ya
miaka hamsini ya Uhuru.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Mh. Dkt. Terezya Huvisa
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Dkt Huvisa aliongeza kwa kusema kuwa, kupitia maadhimisho haya, serikali itapata fursa ya kutathmini hali
ya Mazingira nchini, juhudi mbalimbali zinazofanywa katika kuhifadhi Mazingira, Mafanikio na changamoto
za Mazingira kwa kipindi cha miaka hamsini ya Uhuru.
Aidha, Dkt Huvisa alisema kuwa, Maadhimisho ya mwaka huu yanaambatana na uhamasishaji wa
wananchi wote kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhifadhi Mazingira, kupitia Mikakati mbalimbali na
wananchi pia, wanahamasishwa kuunga mkono utekelezaji wa Mkakati wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi
na Vyanzo vya Maji kwa kushiriki katika mashindano ya Tuzo ya Rais ya Kuhifadhi vyanzo vya Maji,
Kupanda na Kutunza Miti kwa kujaza fomu ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi wakati
wa maadhimisho ya siku ya mazingira ya mwaka 2012 ikiwa ni pamoja na pesa taslimu.
Dkt Huvisa alianisha kuwa, tangu nchi ipate uhuru miaka 50 iliyopita, matatizo ya mazingira nchini
yameendelea kujitokeza akisema kuwa miongoni mwa matatizo makubwa ni pamoja na upotevu na
uharibifu wa misitu ya asili kutokana na kilimo kisichoendelevu, matukio ya uchomaji moto ovyo na ufyekaji
wa misitu ovyo kwa ajili ya shughuli za ujenzi, utafutaji madini na nishati ya mkaa.
Akifafanua zaidi, Dkt Huvisa alisema, taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba takriban hekta za misitu
zipatazo laki nne, hufyekwa na kuharibiwa hapa nchini kila mwaka kutokana na sababu hizo na
kusababisha uharibifu wa vyanzo vya maji na ardhi na aliongeza kuwa, ongezeko kubwa la idadi ya watu
mijini na vijijini limesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa taka na hivyo kusababisha kuzagaa kwa
uchafu na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya mijini na vijijini.
Akifafanua zaidi Dkt Huvisa alisema, Katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru na Siku ya Mazingira
Duniani mwaka huu, wadau wote wa Mazingira ikiwemo Wizara za kisekta, mikoa, taasisi za Serikali,
viwanda, mashirika yasiyo ya kiserikali, kamati za mazingira na kamati za afya za mikoa, serikali za mitaa
na vyombo vya habari, zitumie fursa hii kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu
wa maudhui ya ujumbe wa kitaifa wa maadhimisho haya, hususan kuhamasisha wananchi wote juu ya
kupanda miti na kuhifadhi misitu na uoto wa asili pamoja na kuepuka uchafuzi wa mazingira wa aina
yoyote.
Kitaifa kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni “Miaka Hamsini ya Uhuru,
Kuitunza: Hifadhi Mazingira”

0 comments:
Post a Comment