Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (kulia), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisima cha maji cha Mzinga A kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika eneo la Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam juzi.Kutoka kushoto ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa, Mwenyekiti wa mradi huo, Rashid Nandonde na Meneja Miradi Maalumu wa TBL, Emma Orio.
Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Mary Mbowe, akijaza maji kwenye ndoo baada ya fungulia maji baada ya kuzindua juzi kisima cha maji cha Mzinga A kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika eneo la Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam.
Mkazi wa Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Pili Khamis akifurahi kupata maji baada ya Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (kulia)kuzindua kisima cha maji cha Mzinga A, kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mhandisi Ujenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), John Malisa, akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Josephine Msungwa eneo hilo, Catherine Mwatonoka, wakati wa hafla ya uzinduzi wa kisima cha maji cha Mzinga A, Kisima hicho kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mkurugenzi wa Maji Mijini wa Wizara ya Maji, Mary Mbowe (katikati), ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, akisindikizwa na Meneja Miradi Maalumu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio (kushoto) na Mjumbe wa Kamati ya Mradi wa Kisima cha Maji cha Mzinga A, Kitunda Nyangasa, Dar es Salaam, Lawrence Msyele akitoka kuzindua mradi huo juzi.Kisima hicho kilichojengwa kwa sh. milioni 27 zilizotolewa msaada na TBL.
0 comments:
Post a Comment