Nafasi Ya Matangazo

February 18, 2011

Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba pamoja na Meneja wa mfuko huo Yessaya Mwakifulefule wakishusha na kuwakabidhi vyakula mbalimbali wafanyakazi wa Red Cross waliopo katika kiwanja cha uhuru kwa ajili ya kutoa huduma kwa waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto.

Mkurugenzi wa mahusiano wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwa amebeba  kapu lenye mikate kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru,Vodacom Foundation ilitoa misaada mbalimbali .
 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakishusha vyakula mbalimbali katika lori lililosheheni  misaada  ya  vyakula mbalimbali kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru .
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wa Red Cross wakisaidiana kushusha vyakula mbalimbali katika lori lililosheheni  misaada  ya vyakula mbalimbali kwa ajili ya waadhirika wa janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto waliopo katika kiwanja cha uhuru.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiongea na mmoja wa watoto  waliopotezana na wazazi wao katika janga la ulipukaji wa mabomu Gongo la mboto, akiwa katika kiwanja cha uhuru mara baada ya wafanyakazi hao  kufika hapo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali.
Posted by MROKI On Friday, February 18, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo