Nafasi Ya Matangazo

February 27, 2011

 Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO akizungumza jambo na baadhi ya wateja wa kampuni hiyo walioalikwa wakati wa hafla ya utambulisho wa sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Wasanii wa kikundi cha Splendid Art Group wakionesha umahiri wao  katika mitindo tofauti ya sarakasi wakati wa hafla ya utambulisho wa sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO (kulia) akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Stanbic Bank Bashir Awale sare na mavazi mapya yatakayotumika kuanzia sasa ambayo yana gharama ya shilingi milioni 300 wakati wa hafla ya utambulisho iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Kampuni ya ndege ya Precision Air imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake na kutumia vifaa vyake vya kisasa katika soko la biashara ya ndege pamoja na kujenga muonekano mpya utakaoendana na wakati .

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akizindua sare na mavazi mapya wafanyakazi wa kampuni hiyo, Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Precision Air, ALFONSE KIOKO amesema kwa kuanzia wamezindua mavazi hayo yenye thamani ya milioni 300 yatakayotumika kuanzia sasa.

Akifafanua Kioko alisema sare hizo mpya zimebuniwa na kusambazwa na kampuni ya ushonaji sare ya Boutique New City ya Jijini Bangkok nchini Thailand.

Alisema uamuzi wa kununua sare hizo kutoka nje ya Tanzania umekuja baada ya wabunifu kutoka ndani ya nchi kushindwa kufikia kiwango kilichokua kikihitajika na Precision Air.

“Kuna viwango vitatu vya sare hizo mpya, ya kwanza ni ile ya wafanyakazi watangulizi, pili wafanyakazi watendaji katika ndege, wahandisi na marubani na ya nne ni ya kuvaa katika kazi tofauti za ufundi,”alisema Kioko.

Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege.

Mnamo mwaka 2006 kampuni hiyo na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake.

Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam Septemba mwaka jana. Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) iliwezesha Precision Air kutunukiwa zawadi mbili za kimataifa.

Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.

Kwa upande wake BI MALIALE MINJA ambaye ni mteja wa kampuni amesema kuboreshwa kwa huduma za kampuni hiyo kutasaidia kuleta ushindani katika sekta ya usafiri wa wa anga kwani kampuni zingine nazo hazitakubali kubaki katika hali waliyonayo.
Posted by MROKI On Sunday, February 27, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo