Nafasi Ya Matangazo

December 20, 2010

Baadhi ya Maafisa Habari  Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa pembeni ya Mto Kiwira juzi wilayani Rungwe kwa ajili ya kujionea maajabu ya Daraja la Mungu ambao maji yam to huo yanapita katikati yake. Maafisa hao walifanya ziara ya mafunzo kwa lengo la kujifunza na kujionea kivutio hicho kinavyoweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.
 Muoinekano wa Ziwa Ngosi lilipo katika Milima ya Uporoto. Ziwa hilo linasaidikiwa kutokana na Volcano na maji yake yanachumvi kali na liko katika ya milima mbalimbali.
 Baadhi ya Maafisa Habari  Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa picha ya pamoja mara baada ya kufikia kilele cha Mlima Uporoto ambao unazunguka Ziwa Ngosi. Ziara hiyo ya mafunzo ilifanyika juzi kwa lengo la maafisa hao kwenda kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vya wilayani humo kwa ajili ya kuvitangaza ili visaidie kuongeza pato la Taifa.
 Baadhi ya Watendaji Waaandamizi kutoka Wizara ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo na Maafisa Habari Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa katika Maporomoko ya Malasusa  kwenye Mto Kiwira juzi wilayani Rungwe . Ziara hiyo ya mafunzo ilikuwa ni sehemu ya kikao kazi chao kilichofunguliwa juzi na Waziri wa Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt Emmanuel Nchimbi.
 Mmoja wa Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Pili Rajab akielezea kufurahishwa kwake na maajabu ya baada ya kuona Ziwa Ngosi(nyuma yake) lilipo katikati milima na kulifanya lifanane na Ngorongoro Crater. Mfanyakazi huyo na Maafisa Habari wa Serikali walikwenda Wilayani Rungwe juzi kwa ajili ya ziara ya mafunzo ya vivutio mbalimbali vilivyopo hapo.
Baadhi ya Maafisa Habari  Elimu na Mawasiliano wa Serikali wakiwa pembeni ya Mto Kiwira juzi wilayani Rungwe kwa ajili ya kujionea maajabu ya Daraja la Mungu ambao maji yam to huo yanapita katikati yake. Maafisa hao walifanya ziara ya mafunzo kwa lengo la kujifunza na kujionea kivutio hicho kinavyoweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.
Posted by MROKI On Monday, December 20, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo