Nafasi Ya Matangazo

December 20, 2010

Bi. Harusi mtarajiwa Linda Mshana (kushoto) akiwa na mapmbe wake Grace Msemo siku alipoandaa tafrija ya kuishukuru familia yake na marafiki kwa malezi na sasa anaenda kuungana na mwenza wake wa maisha. Tafrija hii ilifanyika katika ukumbi wa Sunset Twiga Hall Mbezi Beach Dar es Salaam Jumatano Desemba 15, 2010.
Baba wa Linda Mzee Mshana akitoa neno la shukrani kwa wageni wote.
Kiondo Mshana na Mkewe ambao ndio walezi wakuu wa Linda wakiwa ukumbini hapo.
Wadau kutoka Bank M wakiongozwa na Jonson Mshana (kati) nao walikuwepo kumuunga mkono mfanyakazi mwenzao Linda.
Linda akimkaribisha mumewe mtarajiwa chakula kilicho andaliwa siku hiyo na hapa akimlisha aple.
Ilikuwa ni furaha tele kwa kila mtu...
Hawa jamaa ni wachina wa Kipare...ni ndugu wafamilia moja ambao wamefanana sura, sauti maumbo, staili ya uchanaji nywele, uvaaji miwani. Ni baba zake Linda.
Mzee Cleopa David Msuya (waziri Mkuu Mstaafu) alikuwepo sambamba na DC wa Mkuranga, Clament Mshana.
Wageni waalikwa nao walipendeza hawa ni baadhi tu kutoka The Guardian Ltd kwa baba mdogo wa Bi harusi.
Wageni maalum kutoka Ujerumani waliohudhuria tafrija hiyo.
Mapacha hawa waliamua kusakata rumba pamoja ...
...na hawa ni wake zao. Mbele ni mama wa Bi Harusi.
Posted by MROKI On Monday, December 20, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo