Nafasi Ya Matangazo

December 14, 2010


 Baiskeri aliyokuwa anatumia marehemu inavyoonekana baada ya kugongwa ikiwa imehifadiwa katika ofisi ya kiijiji, mwenyewe alifariki hapo hapo mara baada ya kugongwa

 Moja ya magogo yaliyowerkwa barabarani na wananchi

Basi dogo la abiria likiwa limeharibiwa kwenye kioo cha mbele upande wa kulia baada ya dereva wa gari hilo kujaribu kuondoa gari lake mara tu baada ya kutokea kwa ajali hiyo. Basi hilo lilikuwa linashusha na kupakia abiria wakati ajari hiyo inatokea
 Vijana wa Uponda Mkengeni wakiwa na bango linaloeleza kwamba magari yataruhusiwa kupita baada ya kukauka tuta walilolijenga wao huku wakiwa wamesimama juu ya tuta hilo

 Vijana wa Upona Mkengeni wakiwa wamesimama juu ya tuta walilojenga kienyeji kwa kutumia magogo ya miti ya minazi na kuweka mchanga juu yake.
Vijana wakiwa wanacheza mchezo wa drafti barabarani kuonyesha kwamba eneo hilo limebadilishwa matumizi, kwa nyuma yao (hawaonekani pichani) walikuwepo wazee wakiwa wanacheza mchezo wa bao la kiswahili.
Askari polisi wakijiandaa kutumia kutumia nguvu ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi baada ya wanachi kukataa ombi la mkuu wa kituo, hata hivyo mkuu wao aliwakataza baada ya wananchi kusema wataharibu magari kwa mawe



Wananchi wa Uponda Mkengeni Kata ya Mjawa Wilayani Rufiji wamesababisha msurulu wa magari na wasafiri mbalimbali kushindwa kuendelea na safari baada ya kuzuia magari yasipite katika kijiji chao.

Hayo yalitokea jana jioni eneo la uponda mkengeni baada ya kutokea kwa ajali ya gari kumgonga mwanamke mmoja aliyekuwa anaendesha baiskeri katika eneo hilo. Mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana anakadiliwa kuwa na umri wa miaka 40, ni mwenyeji wa kijiji hicho cha Uponda Mkengeni.

Akielezea ajari hiyo, Ndugu Salum Matila alisema ajari hiyo imetokea majira ya saa 10 jioni hapo jana na kwamba mwendesha baiskeri huyo alifariki pale pale mara baada ya kugongwa na gari lililomgonga halikusimama.

Ajari hii ni ya tatu kutokea katika eneo hilo ndani ya mwaka mmoja na ajari mbili zimetokea ndani ya mwezi mmoja hali iliyopelekea wananchi kupandwa na hasira na kuamua kuzuia magari kupita mpaka hapo serikali itakapo wajengea matuta katika eneo hilo.

Awali baada ya ajari ya kwanza kutokea wananchi hao walifanya fujo ya kuzuia magari wakidai kujengwa kwa matuta yatakayofanya magari yawe yanapunguza mwendo katika eneo hilo ambalo lisilo na kona na hivyo kufanya magari kukimbia sana. Serikal ilikubali na ikajenga matuta madogo madogo na kuweka alama za kupunguza mwendo hadi mwendo kadi wa kilomita 50 kwa saa hata hivyo ajari zimeendelea kutokea.

Askari walifika eneo la tukio majira ya saa 12 jioni kufaribu kuwaomba wananchi kuruhusu magari yapite vinginevyo wangetumia nguvu, hata hivyo hali hiyo haikusaidia bali ilichochea zaidi maana wananchi hao wakachoma matairi barabarani na kupiga kelele za kuhamasishana kwamba askari wakianza kuwapiga wao wapige mawe magari ya abiria hali iliyoonekana ingeleta madhara makubwa kwani kutokana na uchache wao wasingeweza kuzuia eneo lote maana kulikuwa na msululu mrefu wa magari karibu mita mia 700, ndipo mkuu wa maaskari akasitisha zoezi hilo.

Wasafiri waliokuwa katika eneo hilo walikerwa sana na kitendo cha viongozi kushindwa kulishughulika mapema tatizo lililokuwa limejitokeza kwani viongozi wa Wilaya hawakuweza kufika katika eneo la tukio mpaka ilipofika saa 2.00 usiku wakati ajali ilitokea saa 10 jioni, hali iliyosababisha kuwa na mashaka kama wangeweza kuunganisha safari kwa kuwa walikuwa wanaenda Mwanza na Msoma.




Posted by MROKI On Tuesday, December 14, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo