Nafasi Ya Matangazo

December 14, 2010

 Mwakilishi wa kampuni ya uwakala wa Bima ya Africa Trade Insurance Agency ( ATI nchini, Albert Rweyemamu kushoto akizungumza na waandishi katika warsha ya kuelimisha soko la hapa nchini juu ya uwekezaji na bima za mikopo ya biashara, Dar es Salaam .
Mwakilishi wa kampuni ya uwakala wa Bima ya Africa Trade Insurance Agency ( ATI nchini, Albert Rweyemamu kushoto akiwaelekeza jambo waandishi wa habari katika semina iliyofanyika ivi kalibuni jijini Dar es salaam ,chini ni Ofisa  Mdhamini mkuu wa kampuni ya Africa Trade Insurance Agency ATI , Stewart  Kinloch.


KATIKA kuhakikisha inaongeza ufahamu kwa kuwafikia wateja wake, kampuni ya Uwakala wa Bima za Uwekezaji na Biashara ya African Trade Insurance (ATI), hivi karibuni imefanya semina kwa ajili ya mawakala, maofisa wa benki na vyombo vya habari.

Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika hivi karibuni kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa semina hiyo, Afisa Mdhamini Mkuu wa ATI, Stewart Kinloch alisema: “Lengo la semina hizi ni kulielimisha soko la hapa nchini juu ya uwekezaji wetu wa kipekee na bidhaa zetu nyingine za bima za mikopo ya biashara.

“Huduma hizi zinaweza kuwalinda wauzaji wa bidhaa nje ya nchi wanaolenga masoko mapya, kulinda mabenki dhidi ya mikopo isiyolipwa pamoja na wawekezaji wanaolenga masoko yasiyo na usalama.”

Mbali ya Kinloch, mwingine aliyetoa somo wakati wa semina hiyo ni mwakilishi wa ATI nchini, Albert Rweyemamu aliyeelezea dhamira ya dhati ya kampuni hiyo katika kuhakikisha inakuwa mfano wa bima `mkombozi'.

Tangu kufunguliwa kwa ofisi yake nchini Aprili mwaka huu, ATI imefanikiwa kukuza biashara zake Tanzania kutoka kiwango cha thamani ya uendeshaji cha dola milioni 11 za Kimarekani mwaka 2009 hadi kufikia zaidi ya dola milioni 195 mwaka huu.

Ukuaji huo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 1,000 na aina hiyo ya bima hunufaisha sekta za nishati, uzalishaji na huduma. Wakala huyo wa bima za aina mbalimbali pia amewezesha uwekezaji hapa nchini kutoka nchi za Canada, Italia na Mauritius, nchi hizo zikiwa zimewekeza nchini zaidi ya dola milioni 24 za Kimarekani.

Katika semina hiyo, wadau wa biashara nchini waliweza kujionea manufaa ya wazi ambayo watayapata kwa kukwamuliwa na ATI pale itakapotokea wamekwama kibiashara.

“Faida ya kipekee ATI iliyonayo ni kwamba nchi za Kiafrika kama Tanzania zimewekeza fedha zao ili kuwa mwanachama wa ATI, na hivyo serikali zao hazina sababu ya kusababisha madai yoyote.

“Wawekezaji wanahakikishiwa usalama na uhusiano huu na wamechagua bima ya ATI badala ya makampuni mengine ya nje ya bara la Afrika makusudi kwa sababu hii ni taasisi ya Kiafrika yenye uelewa mzuri wa changamoto na fursa zilizopo kwenye mazingira ya biashara ya hapa,” alisema Kinloch.

Bima ya mikopo ya biashara ni bidhaa ambayo wauzaji bidhaa nje wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini wamekuwa wakiitumia kwa manufaa makubwa kwa miongo mingi. Wauzaji wa nje kutoka kwenye masoko haya wana bima kutoka mashirika ya nchi zao zinazowalinda dhidi hatari kama vile kutolipwa, zinazowawezesha kufanya biashara popote duniani. Kwa ujumla, hali hii inawafanya wawe na uwezo wa ushindani kuliko wenzao wa Afrika ambao mara kwa mara wanatumia fedha taslimu dhidi ya hati au nyaraka zinazoidhinisha mikopo.
Posted by MROKI On Tuesday, December 14, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo