Nafasi Ya Matangazo

December 18, 2010

 Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akifurahi na watoto yatima wa kituo cha Faraja Arusha mara baada ya kukabidhi misaada.
 Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel akikabidhi misaada kwa watoto yatima wa kituo cha Faraja kilichopo Arusha.
 Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel pamoja na warembo wengine katika picha ya pamoja na watoto yatima katika kituo cha Camp Moses.
 Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel pamoja na warembo wengine wakifurahi na watoto yatima katika kituo cha Camp Moses Arusha.
Miss Tanzania 2010 pamoja na warembo wengine wakiwa na watoto yatima katika kituo cha Mama Kevina Arusha mara baada ya kukabidhi msaada huo.


Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel pamoja na warembo wengine walioshiriki mashindano ya urembo ya Vodacom Miss Tanzania 2010 wapo mkoani Arusha tangu tarehe 15 Desemba 2010 kwa shughuli za jamii ambapo tayari wameshatoa Misaada ya kibinaadamu kwa Vituo vya kulelea watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu mkoani Arusha.

Mrembo huyo ambaye pia amefuatana na warembo wengine 8 akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili kwa mwaka 2010 Glory Mwanga ambaye pia ni Miss ARusha na mrembo anayewakilisha Kanda ya Kaskazini, jana [17-12-2011] wametembelea vituo vitatu ambavyo ni 1) Mama Kevina kilichopo eneo la Kijenge Arusha. 2) Camp Mosses kilichopo eneo la Kwangulelo Arusha, 3) Faraja Centre kilichopo eneo la Kimandolu Arusha.

Warembo hao wote kwa pamoja walikabidhi Vyakula, sabuni, madaftari na kalamu, mafuta ya kupikia, vyandarua, pipi, chokreti, na mwanasesere kwa vituo vyote hivyo ikiwa ni pamoja na pesa taslim kwa kituo cha Faraja ili zisaidie watoto hao ambao wanaishi katika mazingira magumu zaidi kulinganisha na vituo vingine.

Sister Genevieve Joseph wa kituo cha Mama Kevina, alitokwa na Machozi alipokutana na mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel wakati akikabidhiwa misaada hiyo kwa ajili ya kituo chake, alisema hii ni mara ya kwanza katika mwaka huu 2010 kituo chake kupokea aina yeyote ya misaada kutoka kwa wasamaria wema, na aliomba wasamaria wema wengine wajitokeze na kuiga mfano huu.

Tunashukuru kwa Miss Tanzania 2010 na ujumbe wako kuja kututembele leo hii tumepata faraja kubwa na tunamuomba Mungu awajalie muendelee na moyo huo huo wa kusaidia watu wengine wenye shida kama sisi, alisema sister Genevieve Joseph huku akibubujikwa na machozi.

Misaada aliyokabidhi Miss Tanzania 2010 kwa vituo hivyo vina gharama ya shilingi milioni tatu, [3,000,000/-] ziara hiyo katika mikoa ya Arusha na Moshi imedhaminisha na Kampuni ya Ndege Insurance pamoja na Vodacom Tanzania.

Miss Tanzania 2010 pamoja na ujumbe wake wataelekea Moshi Kilimanjaro tarehe 18 Desemba 2010 siku ya Jumamosi kwa shughuli kama hiyo kabla ya kurejea D'salaam siku ya Jumatatu ijayo.
Posted by MROKI On Saturday, December 18, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo