Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Yosefu Goba jijini waliohitimu kidato cha nne wakiwa kwenye maandamano kutoka jengo la bweni lililogharimu milioni zipatazo 300, Jengo hilo lililozinduliwa siku hiyo ya mahafali limejengwa kwa mkopo kutoka Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)
Wanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Mtakatifu Yosefu Goba jijini wakimuonyesha mgeni rasmi wa mahafali ya pili ya kuwaaga kidato cha nne Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bibi Rosemary Lulabuka jinsi wanavyoweza kufanya majaribio mbalimbali ya masomo ya sayansi katika maabara yao.
Mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya kuwaaga kidato cha nne ya shule ya Sekondari Mtakatifu Yosefu Goba, Bibi Rosemary Lulabuka akimpa zawadi Bi Thecla Kisusi ambae ni msichana aliyefanya vizuri katika masomo mengi shuleni hapo.




0 comments:
Post a Comment