Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi na utenguzi wa
viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa na kutenguliwa ni kama
ifuatavyo:-.
(i) Mhe. Patrobas Paschal Katambi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, anachukua nafasi ya Mhe. Boniface George Simbachawene (Mb.) ambaye uteuzi wake umetenguliwa;
(ii) Mhe. Prof. Palamagamba John Aidan Kabudi (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum). Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Prof. Kabudi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo;
(iii) Mhe. Paul Christian Makonda (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Makonda alikuwa Naibu Waziri katika Wizara hiyo;
(iv) Mhe. Dennis Lazaro Londo (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi huu, Mhe. Londo alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi; 2
(v) Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud (Mb.) ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi;
(vi) Dkt. Richard Stanslaus Muyungi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Dkt. Muyungi anachukua nafasi ya Mhandisi Cyprian John Luhemeja ambaye ameteuliwa kuwa Balozi;
(vii) Mhandisi Zena Ahmed Said ameteuliwa kuwa Balozi;
(viii) Bw. Waziri Rajab Salum ameteuliwa kuwa Balozi;
(ix) Meja Jenerali Mbaraka Naziad Mkeremy ameteuliwa kuwa Balozi;
(x) Mhandisi Ally Samaje ameteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST). Mhandisi Samaje anachukua nafasi ya Dkt. Mussa Daniel Budeba; na
(xi) Uteuzi wa Prof. Eliakimu Mnkondo Zahabu, Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) umetenguliwa.
Aidha, uapisho wa viongozi wateule utafanyika tarehe 13
Januari, 2026 Ikulu Chamwino, Dodoma kuanzia saa 8.00 mchana.





0 comments:
Post a Comment