Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar unavyoonekana kwa mbele ukishuka na ndege uwanjanai hapo.
Hapa ni sehemu ya kupumzikia abiria wakati wakisubiri ndege, juu katika dari ndo kama unavyoona na huu ni Uwanja wa Kimataifa. Wahusika mpo wapi kurekebisha uwanja huu na ukaonekana kweli ni wakimataifa. Abiria ambao wengi wao ni wageni toka nchi za Ulaya na Asia wakisubiri ndege Uwanjani hapo. Mbali na kuharibika paa lakini hakuna viyoyozi katika uwanja huo ambavyo vinafanya kazi ipasavyo. Mapato yanayopatikana kutoka kwa ushuru wa wageni hawa kuingia Kisiwani Zanzibar yangekuwa yanatumika pia kufanyia ukarabati uwanja na si kusubiri wanao tangaza kutupakia rangi. Moja ya ndege kubwa ziletazo watalii maelfu kwa maelfu Kisiwani Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment