Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2010

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Capt. George Huruma Mkuchika (pichani) amepita katika kura za maoni na kuwatupa wapinzani wake wawili Juma Abdalah SadicManguya na Rashid Akibar Namwangala katika kura za maoni ya kutafuta Mgombea Ubunge wa Jimbo la Newala kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu utakao fanyika Oktoba 31 2010 nchini kote.


Matokeo hayo yaliyotangazwa muda si Mrefu na Katibu wa CCM Newala ambaye ndiye Mkurugenzi na Msimamizi wa Uchaguzi huo Alexandria Katabi, alisema Mkuchika amepata kura 9,648, Akibar 6,595 na Manguya 5,341.



Aidha habari kutoka Newala zinasema Manguya katika hali ya kushangaza aliitisha mkutano wa tathmini na wapambe wake na kuwanyang'anya pikipiki alizowapa wapambe hao kwa lengo la kufanikisha ushindi kwake.


(
Posted by MROKI On Tuesday, August 03, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo