Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2010

Makundi ya watu wenye ulemavu yakijitokeza kuunga mkono juhudi za Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu leo jijini Dar es salaam.
Vijana wa CCM kutoka vyuo vikuu wakifurahia zoezi la uchukuaji fomu mgombea Urais Dkt Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.

Mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Mohammed Gharib Bilal akiongea na wananchi na wanachama wa CCM leo mara baada ya Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwaonyesha fomu ya kugombea Urais wanachama mbalimbali waliojitokea mara baada ya kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam. Picha no 8. Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi mara baada ya kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua fomu ya Urais leo jijini Dar es salaam.

Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Dkt Jakaya Kikwete(katikati) akishirikiana na wanachama na viongozi mbalimbali wa CCM kuimba nyimbo mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi leo wakati wa kuchukua fomu tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam ambao pia ni wanachama wa CCM wakielekea zilipo ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumsindikiza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Jakaya Kikwete kuchukua fomu leo jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa akizungumza jambo na Mgombea mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dkt Mohammed Gharib Bilal wakati wa kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya kugombea Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete akiwa na Mama Maria Nyerere leo katika viwanja vya ofisi ndogo ya CCM ya Makao makuu Dar es salaam tayari kumsindikiza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. Jakaya Kikwete kuchukua fomu ya kugombea Urais Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Kutoka kushoto ni Mgombewa Mwenza wa Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Mohyamed Gharib Bilal, Rais Jakaya Kikjwete ambaye pia ni Mgombea Urais wa CCM, na Katibu Mkuu wa CCM Yusufu Makamba wakiwa katika mkutano huo baada ya kutoka kuchukua fomu.

Posted by MROKI On Monday, August 02, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Watanzania lini tutabadilika? hivi utamwitaje Kikwete Dr? Watanzania tujifunze kutumia titles stahili. Unafiki tuweke pembeni. Sidhani kama watu wanaelewa dhana halisi ya mtu kupewa title hi ya Dr. !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo