Nafasi Ya Matangazo

August 02, 2010

Kamishna wa Kamisheni ya Operesheni ya Jeshi la Polisi Paul Chagonja akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake kutoka kwa askari wa Polisi Wilaya ya Magu wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa kuona namna ambavyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linajiandaa kwa kusimamia uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Kamishna Chagonja yuko katika ziara ya Ukaguzi wa Polisi Mkoani Mwanza pamoja na kuangalia maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huuu kwa upande wa Ulinzi na Usalama. Kamishna wa Kamisheni ya Operesheni ya Jeshi la Polisi Paul Chagonja (kushoto) akipokea msaada wa Computer pamoja na vifaa vingine kutoka kwa Meneja Miradi wa Shirika la Kimataifa la Planning Mkoa wa Mwanza, Bw. Daniel Kalimbia. Vifaa hivyo ni kwa ajili ya Kikosi cha Mbwa na Farasi mkoa wa Mwanza kwa ajili ya uwekaji kumbukumbu za walimu wa somo la Usalama Wetu kwanza linalofundishwa na askari Polisi katika baadhi ya shule za msingi nchini hapa nchini. Kamishna wa Kamisheni ya Operesheni ya Jeshi la Polisi Paul Chagonja akisalimiana na mmoja wa kazi wa Kijiji cha Nyamikoma Wilaya ya Magu mkoani Mwanza mara baada ya kukagua shughuli za Ulinzi Shirikishi katika Wilaya hiyo pamoja na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji hicho. Kamishna Chagonja yuko katika ziara ya Ukaguzi wa Polisi Mkoani Mwanza pamoja na kuangalia maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huuu kwa upande wa Ulinzi na Usalama.
Posted by MROKI On Monday, August 02, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo