Nafasi Ya Matangazo

July 25, 2010

Mwandishi wetu
Moses Omuteku meibuka bingwa wa mashindano ya mchezo wa gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya gofu vya Lugalo vya jijini Dar es Salaam baada ya kupata pointi 37 na kumzidi Walui Mwangi ambaye pia alipata pointi 37 lakini tofauti ilikuwa katika viwango vya uchezaji.

Mashindano hayo ambayo ufayika kila mwisho wa wiki katika viwanja hivyo na kudhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania, yalikuwa na upinzani mkali kwa kila mshiriki kuonyesha kiwango cha juu cha uchezaji.

Kufuatia ushindi huo Omuteku alizawadiwa seti ya vyombo vya ndani na zawadi nyingine kutoka Zain.

Wachezaji wengine ambao walishinda na kuzawadiwa zawadi na Zain ni Hassan Nkya, Rafael Letara, David Muthungu na Ayne Magombe.

Wiki ijayo mashindano hayo yatawashirikisha wachezaji kutoka nje ya mkoa wa Dar es Salaam, hali ambayo baadhi ya wachezaji wa klabu hiyo wamesema kuwa itaongeza ushindani mkubwa.

Meneja wa uhusiano wa Zain Tanzania Muganyizi Mutta alisema kuwa wao kama wadhamini wakuu michuano iyo wamepania kuboresha zawadi kama changamoto kwa washiriki.

“Sisi tunafurahi sana kuona vijana wengi wanajitokeza katika mchezo huu na kwa maana hiyo basi sisi kama wadhamini wakuu wa mchezo huo wa gofu tumeboresha zawadi ambazo nisingetaka kuzitaja kwa sasa hivi,” alisema Mutta

Klabu ya gofu ya Lugalo mpaka sasa imeishatoa wachezaji bora ambao wamekuwa wakishiriki mashindano ya gofu ya kitaifa na kimataifa na kuonyesha kiwango kizuri na kinachokubalika katika mchezo huo.
Posted by MROKI On Sunday, July 25, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo