Nafasi Ya Matangazo

July 09, 2010

Mwanamuziki wa muziki wa Kizazi kipya Bongofleva Selemani Msindi anayejulikana kama Afande Sele akiimba kwa hisia wakati wa tamasha la Sabasaba Concert lililoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke Julai 6-7 ambapo wasanii mbalimbali walishiriki ikiwa ni pamoja na bendi za muziki wa dansi.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yesaya (AY) akifanya vitu vyake jukwaani wakati wa tamasha hilo” Sabasaba Concert “ lililoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na kufanyika kwa siku mbili mfululizo Julai 6-7 kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke, tamasha hilo lilishirikisha wasanii wa mbalimbali pamoja na bendi za muziki wa dansi.
Wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact wakicheza jukwaani wakati wa tamasha la “Sabasaba Concert “ ambalo liliandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke jijini Dar es salaam lililoshirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya na bendi za muziki wa dansi.
Umati mkubwa wa watu ulijitokeza katika tamasha la Sabasaba Concert lililoandaliwa na Vodacom Tanzania ambapo watu wananchi walijipatia furusa ya kununua simu kwa bei nafuu na kuweza kusajili laini za simu zao pia .
Vijana hawa wakighani kwa staili inayojulikana kama”Kumchana Mwezio”wakati wa tamasha la Vodacom lililojulikana kama Sabasaba Concert kwenye viwanja vya Mwembeyanga wilayani Temeke ambalo lilifanyika kwa siku mbili mfululizo na kushirikisha wasanii mbalimbali zikiwemo bendi za muziki wa dansi.

Posted by MROKI On Friday, July 09, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo