Baadhi ya Bendera za mataifa mbalimbali zaidi ya 15 yanayoshiriki maonesho ya 34 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam zikipepea nje ya Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere Dar es Salaam.Ikiwa ni siku ya pili ya maonesho leo lakini bado idadi ya watu waingiao katika maonesho hayo ni ndogo. Baadhi ya wakzi wa Dar es Salaam wakiangalia moja ya vifaa vya nyumbani vya kutengenezea juice na mambomengine toka banda la Singapore. Kutoka C&C watengenezaji wa dawa za Meno za Whitedent nao walikuwepo na watoto wanafurika na wazazi wao. Mzee wa madekio nae katia timu tena kama kawaida. Wanaume nao walishiriki kuangalia vitu vya nyumbani... Mzee wa Sumo na mwenzake Zuma waliona bora wafanye mazoezi ya kutekenya mwili kwa banda la Singapore. Siku ya pili bado wateja si wengi hadi jamaa akaamua auchape usingizi na kawaida ukilala na biashara nayo inalala. Mkazi wa Dar es Salaam akipita karibu na vitu ambavyo vimewekwa nje katika maonesho hayo. Maonesho ya mwaka huu yamekosa uchangamfu uliozoeleka kutokaka na kuongezeka kwa gharama za upangaji jambo lililopelekea makampuni mengi na baadhi ya wajasiriamali kukosekana viwanjani humo.
0 comments:
Post a Comment