Nafasi Ya Matangazo

May 28, 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkurugenzi Mwenza wa Taaisi ya ADEA Doglas Mcfalls (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari Dar es Salaam jana juu ya maonesho ya vitu vya utamaduni vya makabila ya Makonde, Makua na wayao yajuliknayo kama MAKUYA yaliyoanza jana hadi Juni 12 mwaka huu katika ukumbu wa Alliance Francaise Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza wa ADEA Philipo Luhale.

Taarifa ya “Tamasha la ngoma za asili MaKuYa 2010
Taasisi ya ADEA “ The Center For African For African Development Through Economics & Te Arts” inayo furaha kuujulisha umma tamasha la tatu la “MaKuYa” kuwa litafanyika wilayani Masasi kuanzia tarehe 30/07/2010 hadi tarehe 1/08/2010.
Kama mnavyojua, tamasha la MaKuYa ni jitihada za taasisi isiyokuwa ya kiserikali ADEA ambayo imekuwepo mkoani Mtwara tangu mwaka 2003 kusaidia wasanii (wachonga vinyago vya kimakonde,mafundi chuma,wasusi vikapu,wachoraji na mafundi cherehani) kupitia maafunzo yanayowasaidia kusisimua ubunifu na utafutaji wa masoko ya bidhaa zao.



Kwa nini MaKuYa?


Kw a karne makabila kusini mwa Tanzania yamekuwa yakicheza kwa siri,na kupelekea kuendelea kuwepo kwa utamaduni wa pekee wa sanaa ya kucheza,ambayo imejificha kutoka uso wa dunia hadi sasa. Hata hivyo, jinsi wimbi la utandawazi linavyoendelea kuvamia bara la Afrika, tamaduni hizo za pekee ziko katika hatari ya kutoweka kabisa. Bila kuwepo jitihada kama za MaKuYa kusaidia kukuza uelewa wa kitaifa na kimataifa, tamaduni hizi zitatoweka kabisa katika kizazi hiki.


Kwa kutimiza lengo endelevu,MaKuYa kwa mara nyingine itawaleta pamoja wasanii kutoka vijijini katika wilaya tano za mkoa wa Mtwara. Tofauti na tamasha la kwanza na lile la pili ambayo yalifanyika katiak manispaa ya Mtwara Mikindani, mwaka huu tamasha litafanyika katika wilaya ya Masasi. Badiliko hili la mahali pa kufanyia tamasha litatoa fursa zaidi kwa wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mtwara kushuhudia uwepo wa uchezaji na utamaduni wa watu wa huko.



Tamasha la MaKuYa litawaleta pamoja wasanii kutoka katika makabila ya wamakonde,Wamakua na Wayao; makabila makubwa ya mkoa wa Mtwara. Zaidi ya wasanii wacheza ngoma 500 wanatarajiwa kujumuika pamoja na kusherehekea utamaduni wao. Wageni watafurahia kutazama michezo ya jadi na kuona maonyesho ya vitu vya asili vya utamaduni vinavyo/vilivyotumika katika maisha ya kila siku.


Mkoa wa Mtwara umekua ukijulikana kwa watu wengi kuwa ni sehemu yenye maisha a ghali sana ambavyo yenye haina vitu vya kutosha kutoa kwa wageni. Tamasha la MaKuYa limethibitisha inalipa kutembelea mkoa huo.


Tamasha la MaKuYa limegawanyika katika sehemu tatu:
1. Uchezaji ngoma za asili
2. Maonyesho ya michezo ya jadi
3. Maonyesho ya vitu vya asili kuonyesha maisha ya jadi ya wananchi.
Aims of this festival are:
Madhumuni ya tamasha la MaKuYa ni kama yafuatavyo:
Kusaidia kuhakikisha uhifadhi endelevu wa ngoma za asili (sanaa ya kucheza na kupiga)

Kuhimiza ngoma za asili (kupiga na kucheza) kwa kutoa jukwaa la vikundi kuchezea kila mwaka.

Kuthibitisha na kutia moyo uchezaji wa ngoma za asili
Kuwezesha vijana kutambua utajiri wa urithi wao wanapokumbwa na
mageuzi ya kisasa.

Kukuza uelewa kwa watu wa Mtwara juu ya urithi utajiri wa sanaa ya kucheza katika ngazi ya jamii,kitaifa na kimataifa.

Kutambulisha umma kuwa ngoma za asili bado zinadumishwa katika eneo

la kusini mwa Tanzania.

Kuwezesha vikundi vya wasanii kukutana na kubadilishana mawazo miongoni mwao.

Kuongeza shughuli za maisha ya kila siku kwa kukuza utalii wa kiutamaduni katika mkoa ambayo itapelekea ongezeko la fursa za kibiashara kwa wenye majumba ya kulala wageni,wasafirishaji,wapika vyakula na wafanya biashara ya zawadi n.k.

Kukuza uelewa na mapenzi kwa eneo la kusini mwa Tanzania.

MAONYESHO YA MaKuYa Dar-Es_Salaam

Maonyesho ya MaKuYa Dar-Es-Salaam ambayo ni utangulizi wa tamasha la MaKuYa litakalofanyika Masasi mwaka huu, yatafanyika kati ya tarehe 28/05/2010 hadi tarehe 12/06/2010 katika katika ukumbi wa Alliance Fracaise. Ni nafasi ya kuwahabarisha wale wote watakaokosa nafasi kuja katika tamasha. Maonyesho hayo yatahusisha picha za mnato,mahojiano na wazee wa makabila ya wamakonde na wamakua kupitia picha za video,vitu vya sanaa, (vinyago vya kuvaa usoni) n.k.

Tungependa kuwashukuru Ubalozi wan chi ya Ufini,Ubalozi wa Uholanzi ambao ndio wafadhili wakuu wa tamasha mwaka huu,( Pia ubalozi wa Uswiss kwa ufadhili wao muhimu tangu kuanza kwa tamasha la MaKuYa) Tungependa pia kushukuru Hotel ya Southern Sun, Alliance Francaise wote wa DSM na Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi kwa misaada yao ya mara kwa msaada wao wa hali na mali.


Tunaishukuru serikali ya Tanzania kupitia chombo chake cha Baraza La Sanaa Tanzania (BASATA) kwa msaada wao usiokoma kuwezesha MaKuYa kufanyika.
Posted by MROKI On Friday, May 28, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo