Nafasi Ya Matangazo

May 03, 2010

Wanafunzi wa Sule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wakimsikiliza mwalimu wao Maua Rashidi (hayupo pichani) kabla ya kushiriki michezo mbalimbali leo shuleni hapo wakati wa kampeni ya kutokomeza Malaria nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi wa shule hiyo kupitia michezo.
Mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka(katikati) Kushoto ni Bw. Godfrey Boniface Afisa kutoka Right to Play Tanzania na kulia ni Bi. Anna McCartney-Melstad Mshauri wa “Voices for Malaria Free Future II – Tanzania kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Bloomberg. Mwanamuziki mkongwe wa Afrika Kusini Yvonne Chaka Chaka(kushoto) ambaye pia ni Balozi wa Kimataifa katika Mapambano dhini ya Malaria Duniani akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya kutokomeza Malaria Duniani yenye kauli mbiu “Tuungane Kutokomeza Malaria” leo katika shule ya Msingi Uhuru Wasichana jijini Dar es salaam.Pamoja na na mambo mengine balozi na mwanamuziki huyo amehimiza ushiriki wa jamii nzima hasa wanafunzi kupitia shule zao kupewa elimu kuhusu Malaria kupitia michezo mbalimbali, Kulia ni Bi. Anna McCartney-Melstad Mshauri wa “Voices for Malaria Free Future II – Tanzania kutoka Chuo cha Afya ya Jamii Bloomberg.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza nguo cha mkoani Arusha cha A to Z ambacho pia kinatengeneza vyandarua akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari kwa kushirikiana na Bi. Yvone Chakachaka namna kampuni ya A to Z inavyoshiriki katika kampeni ya kutokomeza Malaria kwa kutengeneza vyandarua bora na vyenye viwango leo.
Posted by MROKI On Monday, May 03, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo