Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania Kihara Maina (kulia) akikabidhi mpira na bendera kwa nahodha wa timu ya soka ya Barclays Tanzania, Deogratius Ishenda inayokwenda Uingereza kushiriki katika mashindano ya soka ya siku moja yatakayofanyika katika Uwanja wa nyumbani wa mabingwa wa Ligi ya Uingereza, timu ya Chelsea. Mashindano hayo yatashirikisha timu kutoka katika nchini ambazo benki hiyo inatoa huduma zake lengo ikiwa ni kuwafanya wachezaji hao kuweza kujionea wenyewe fahari ya ligi hiyo inayodhaminiwa na Barclays.
0 comments:
Post a Comment