Nafasi Ya Matangazo

May 04, 2010

Athuman Hamisi.
Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Serikali la HABARILEO, Athumani Hamisi ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa anataraji kurejea nchini siku ya Jumamosi Mei 8, 2010.
Kwamujibu wa Chama cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT), ambapo Hadi Machi mwaka huu alikuwa akikitumikia Chama hicho akiwa Mwekahazina Msaidizi, Hamisi atawasili majira ya Saa 12 jioni na Ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Ndugu, Jamaa na marafiki wote wa Athumani Hamisi Msengi wanaombwa kufika katika mapokezi hayo na kumkaribisha tena nyumbani baada ya kuwa mbali kwa kipindi kirefu.
Athumani pamoja na wapigapicha wenzake wawili Anthony Siame na Marehemu Herry Makange walipata ajali ya gari Desemba 12 2008 baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupinduka wakiwa njiani kuelekea Kilwa Masoko Mkoani Lindi kikazi.
Blogu ya watu inamkaribisha Nyumbani Athumani Hamisi .
Blogu ya
Posted by MROKI On Tuesday, May 04, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Nilipata bahati ya kuonana na Bw Athuman wakati akiwa hospitali Jijini Johannesburg.
    Amepata nafuu kubwa sana katika matibabu yake na Bw. Athuman alionyesha nia kubwa ya kutaka kurejea katika hali ya awali kabla ya ajali na pia alikuwa na mipango mingi kuhusu maisha yake ya baadaye.
    Sintakuwa kijijini Jozi kumwaga lakini namtakia kila la heri katika jitihada zake ka kurejea katika hali ya kawaida. Karibu sana Tanzania Bw Athuman
    Mdau
    Dk Faustine

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo