Unyama na ukatili wanaofanyiwa walemavu wa ngozi (Albino) nchini Tanzania bado unaendelea licha ya serikali na mashirika mbalimbali ya Haki za Binadamu Duniani kupiga kelele.
Juzi Mtoto wa Kike Mkazi wa Kijiji cha Luhaga, Kata ya Igwamanoni Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Kabula Nkalango alikatwa mkono wa kuume na watu wasio julikana na kuondoka nao.
Unyama huu hadi lini? Hivi Sisi binadamu tumeumbwabwe tunaroho za namna gani maana hata za kinyama hazifananii.
Uliona wapi mnyama Chui/Simba kamuua Chui Mwenzake au Simba mwenzake.
Inasikitisha. Mungu mbariki Kabula na Albino wote Tanzania uwalinde.




0 comments:
Post a Comment