Nafasi Ya Matangazo

February 12, 2010

Mrembo aliyeshikataji la Miss Tanzania Vodacom 2009, Miriam Gerad leo alipandishwa katika mahakam aya Hakimu Mkazi Kinondoni akiwa mshitakiwa wa pili katika kesi inayomkabili ya Kushambulia na kudhuru mwili pamoja na kuharibu mali zenye thamani ya shilingi 720,000 mali ya Shabani Mushi ambaye ndie walimjeruhi.

Miriam alikumbwa na mkasa huo Usiku wa Februari5 mwaka huu, akidaiwa kuwa na mtu anaedaiwa kuwa ni mpenzi wake Kennedy Vitor (mwenyenguo nyekundu) wakiwa katika burudani Mikocheni Dar es Salaam na kukamata wakiwa pamoja leo asubuhi baada ya msako wa siku kadhaa.

Watuhumiwa hao wote walikosa wadahamini wa kusaini bondi ya dhamana ya shilingi Milioni 1 kila mmoja na kupelekwa mahabusi hadi Jumatatau iwapo taratibu za dahaman zitatimizwa.

Miriam na Kennedy wakirushwa mahabusu baada ya kusomewa kesi yao hadi Februari 25 itakaposomwa tena baada ya uchunguzi kukamilika.
Posted by MROKI On Friday, February 12, 2010 1 comment

1 comment:

  1. jamaniiii eeeee hili balaa sasa pamoja na usupastar wao wanakosa udhamini.kazi ipo kwei kwei yangu macho naomba nimdhamini huyo binti missio 2009.

    mdau boxi 4 laifu

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo