Nafasi Ya Matangazo

February 15, 2010

Bei ya bia zinazotengenezwa na viwanda vya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)kuanzia kesho watalazimika kujikamua zaidi ili kupata kinywaji hicho. Hali hiyo inatokana na TBL kutangaza kupandisha bei ya kinywaji chake – bia.
Taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, ilisema nyongeza hiyo haitazidi Sh 100 kwa kila bidhaa.
Ilisema uamuzi wa kupandisha bei ya kinywaji cha TBL umetokana na ongezeko la gharama za uzalishaji
zikiwamo za malighafi, usafiri, mafuta na kiwango cha kubadilisha fedha.
Baadhi ya bia zenye ujazo wa mililita 500 zilizokuwa zikiuzwa mtaani Sh 1,300 sasa zitauzwa Sh 1,400 ambazo ni Safari Lager, Kilimanjaro, Bingwa, Ndovu Special Malt na
Balimi. Bia zenye ujazo wa mililita 330 ambazo zitauzwa Sh 1,200 kwa rejareja ni Safari Lager, Kilimanjaro na Tusker Lager.
Hata hivyo, hadi jana, bia hizo zilikuwa zinauzwa kwa kati ya Sh 1,400 hadi Sh 1,500 katika baa za kawaida bila kujali ujazo wa kinywaji.
Hii inamaanisha kuwa inawezekana kabisa bei ya kinywaji hicho ikapanda hadi Sh 1,600 kwa chupa au kopo kwa mteja wa kawaida wa rejareja.
Chanzo-HABARILEO
Posted by MROKI On Monday, February 15, 2010 2 comments

2 comments:

  1. Bongo kwa mitambo ya bia tu wameshinda, watu wanaweka mitambo ya maana kwlei tutafika jamani...!!!??

    ReplyDelete
  2. dah cjui itakuaje,ila wanywaji najua hatuna jinsi nikuzishwa tu.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo