Hatimaye kamati ya Miss Tanzania kupitia Mkurugenzi wake Hashim Lundenga leo imefanikio kumtoa mahabusi Miss Tanzania 2009. Miriam Gerald ambaye alikuwa mahabusu tangu Ijumaa Februari 12, 2010.Lundenga aliyeanza pilikapilika za kufanikisha dhamana hiyo iliyowekwa katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kinondoni jana na hatime leo majira ya saa sita mchana mrembo huyo aliachiwa huru akisubiri siku ya kuendelea na kesi ya kushambulia na kuharibu mali inayo mkabili Miriam pamoja na mtu wake wa karibu Kernnedy Victor.
Akitoka kwa mlango wa uwani ili kukwepa Camera za wapigapicha Miriam alishindwa kutimiza adhma hiyo na kujikuta akikutana uso kwa uso na wapigapicha za habariwakati akitafuta mlango wa kutokea nje ya uzio Mahakamini hapo leo.
Siku akienda mahabusu Miriam alifanikiwa kupata khanga na fulana kubwa kutoka kwa kijana ambayeni rafiki yake na kujifunika licha ya kuwa tayari Alisha pigwa picha hizo mapema zaidi.
Miriam anafanya orodha ya waremba wawili wa Miss Tanzania kwa miaka ya 2008 na 2009 wanaofikishwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za ugomvi huku wakwaza akiwa ni Wema Sepetu aliyetuhumiwa kuharibu mali ya msanii Kanumba.






0 comments:
Post a Comment