Nafasi Ya Matangazo

January 19, 2010

Ajali za barabarani zinaendelea kupukutisha maisha ya watanzania na kupoteza mali ambazo zinachumwa kwa juhudi kubwa.Ajali hii imetokea jana( leo) katika barabara ya Morogoro, maeneo ya Mdaula ambapo lori lililokuwa na magunia ya ngano yenye lakiri ya Azam lilipogonga kwa nyuma lori la mafuta la kampuni ya Kobil lililokuwa na mafuta ya dizeli.Mtu mmoja anayeaminika kuwa tanboi alifariki papo hapo baada ya kebin ya lori lenye unga kusambaratishwa kabisa.dereva hali yake inadaiwa ni mbaya.polisi waliwahi kufika kuzuia watu kupakua mafuta na ngano ambazo kiasi fulani imemwagika lakini nyingi ikiwa bado katika lori lenye tela namba T 373 ASF ambalo kebin yake T492 ASE ilisambaratishwa.Chanzo cha ajali hakijajulikana na polisi waliokuwa hapo walikataa kusema kwa kuwa wao si wasemaji.Mafuta kutoka katika lori namba T912 AZU yalikuwa yanaendele akumwagika hadi saa sita mchana jana.
HABARI ZA HIVI PUNDE ZINA PASHA KUWA KUN AAJALI IMETOKEA KIBAMBA NA WATU ZAIDI YA KUMI WANAHOFIWA KUFA.
Posted by MROKI On Tuesday, January 19, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo