
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu katika Manispaa ya Moshi (MMFA), Abuu Mrutu, (wa pili kulia), akipokea mipira kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya Kombe la Chifu Marealle, Hassan Kaniki, ikiwa ni sehemu ya mipira itakayotumika katika mashindano hayo, yanayoendelea mjini Moshi. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mjini Moshi jana, ambayo ilijumuisha na kukabidhi zawadi mbali mbali zitakazokabidhiwa kwa timu zinazoshiriki mashindano hayo, ambayo yanathaminiwa na Kampuni ya Bia ya East African Breweries Limited.

Mwenyekiti wa Ukoo wa Marealle, Dk. Wilfred Marealle (wa pili kulia), akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Kombe la Chifu Marealle, Hassan Kaniki, ikiwa ni sehemu ya zawadi zitakazotolewa kwa timu zinashiriki mashindano hayo, vyenye thamani ya sh 11.1 milioni, katika hafla iliyofanyika mjini Moshi jana. Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya Executive Solutions na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya East African Limited.
0 comments:
Post a Comment