Familia ya Bwana na Bibi Onesmo Nathan wa Kimara Bucha Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao Kipenzi Diana Onesmo Nathan kilichotokea leo katika Hospitali ya Herbert Kairuki Dar es salaam.
Mipango ya mazishi inafanyika Kimara mwisho kwa Mzee Kaluse.
Mipango ya mazishi inafanyika Kimara mwisho kwa Mzee Kaluse.
Poleni kwa msiba!
ReplyDeleteDiana umeondoka lakini tunaimani upo pema!
jamani Mroki Mroki mtoto kaugua nini? mbona kama ghafla sana au kalizaliwa na matatizo? inasikitisha halafu inauma sana malaika kama huyo kutoweka duniani tena kwa muda mchache tu baada ya kuiona dunia. wazazi poleni sana na mtegemeeni Mungu kwani ndio yeye aliyewapa na ndiye alieamua kumchukua. muombeeni apumzike kwa amani milele. RIP Diana lovely
ReplyDeletePole sana Onesmo kwa msiba mzito ulokupata. Inanikumbusha miaka mitatu ilopita kaka yangu alifiwa binti yake siku alotimiza mwaka mmoja. Kwakweli tuliumizwa sana sana.
ReplyDeleteHuwa nasikitishwa sana na hivi vifo vya watoto wadogo, lakini ndo hivyo tena sie binadamu hatuna amri kwa hilo.
Uwe na moyo wa uvumilivu nikweli ni huzuni kubwa, ila kumbuka sisi wote twapita tu hapa duniani.
Wewe ulimpenda lakini mungu kampenda zaidi na jina la bwana lihimidiwe.
Bwana alitoa na bwana ametwaaa jina la Mungu lihimidiwe.
ReplyDeletePoleni kwa msiba mrocky..
Jane
Diana Onesmo. Mungu amekuita malaika wake ukiwa bado mdogo. Yote hiyo ni mipango yake kwani Yeye ndiye Anajua. Japo umewaachia uchungu mzito usioelezeka wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zako, wote wanafarijika kujua kwamba Mungu amekuita na kwake uko kwenye furaha na amani ya kweli. Pumzika salama Diana.
ReplyDeleteRIP Diana. Sikupata kukufahamu lkn nimeguswa. Poleni wazazi.
ReplyDeletePoleni sana kwa msiba, masikini mtoto alikuwa mzuri, nimepatwa na simanzi kubwa. Poleni sana na Mungu awajaze nguvu ktk kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteKwa mzazi yeyote hakuna unalohitaji kuelezwa kuelewa uchungu wa kuondokewa na mwanao. Na hasa baada ya pilika zoote za malezi ya ndani na mpaka anapozaliwa na kuwa alivyo. Na wakati mwingine inakuwa ngumu kupata jibu la kwanini Mungu ameamua kumuita mapema namna hiyo. Lakini hakuna asiyejua kuwa Mungu anatenda yaliyo sahihi kiImani japo kimwili twaweza kuona si sahihi. Mungu kampenda zaidi na zaidi ya yote ameendelea kuwapa faraja wazazi, walezi na jamaa za Diana.
ReplyDeleteBasi kwa wakati huu ni kumshukuru na kumuomba Mungu aendelee kuwa kiongozi kwa familia. Kutambua kuwa kama ametenda, ni kwa kuwa anajua tunaweza kuhimili na tunaweza kuendelea kumtukuza. Na sasa tusifunge baraka zake kwa kupungukiwa imani. Tuendelee kuamini kuwa tuna nafasi ya zaida kwa sasa na wakati ukifika tutaitwa pia. Diana ameondoka akiwa mchanga na twaamini yuko mahala pema, nasi tuendelee kutenda yaliyo mema kwani ndio njia pekee ambayo itatukutanisha naye na kuwa na furaha ya milele pamoja naye.
Amani na upendo kwa wote
Poleni sana na msiba huu!
ReplyDelete