
Mgambo wa Manispaa ya Ilala wakianglia meza ya magazeti mtaa wa Samoro Dar es Salaam Agosti 12 2009 leo, siku moja baada ya mkuu wa Mkoa kuwataka wavae vitambulisho na wafanye kazi za muhumu na sio kukimbizana na mamalishe.

Mgambo wakiondoka baada ya kuona wanapigwa picha walipokuwa wakitaka kumkamata muuza magazeti kwa kosa la kuuza vitabu vya riwaya.

Mgambo aliyetambulika kwa namba MG 364163 -Salvatory Tutus Mkalava mkazi wa Kitunda Dar es Salaam, akionyesha nakala ya kitambulisho chake ambacho hakina nembo ya Jiji au mamlaka anayofanyia kazi. Mgambo huyu alikuwa na wenzake wanne walipoona mwenzao ametoa kitambulisho kisichona sifa wakatoweka. Blogu hii ya jamii inatoa tahadhari kwa watu wa namna hii maana wengine ni wahalifu wanaovalia sare za mgambo na kubeba vitu vya wanyonge.
Kweli mamlaka za jiji hazina habari na wanachi na hao mgambo wao. Kwanini wanatoa ruhusa kwa mgambo kufanya kazi bila kuwa vitambulisho kamili?
ReplyDeleteHali ya sasa sio nzuri watu wanatafuta hela kinguvu, na wanachi wanadhurika kila kukicha na hata hao mgambo feki wanapatiwa kibano mara nyingine, sasa kwanini wahusika msifatilie swala hili la kila mtu awajibike kihalali?
Kweli mtu anathubutu kuonesha kitambulisho feki na akiwa na uniform? Sasa tumwamini nani????
Wakubwaeeee kuweni na utu! Nikitu kidogo tu kutoa vitambulisho kwa waajiliwa wenu.