Nafasi Ya Matangazo

August 24, 2009

Morani wa Kimasai wa kijiji cha Kimokouwa kata ya Namanga wilayani Longido wakiokoa mifugo yao iliyozama katika dimbwi la maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juzi kijijini hapo na kusababisha mifugo mingine kufa. Ng'ombe hao walikuwa wanakunywa maji lakini walishindwa kutoka kutokana na kukosa nguvu. Vijana hao toka kulia ni Roymen Kayongo, Philipo Saroni na Samueli Molel. Hii ilikuwa Marchi 1 2006.
Kwa wafugaji ilikuwa ni janga kubwa. mfugaji aliye na Ng'ombe elfu 3 alibaki na kumi au chini ya hapo wengine walikufa.
wafugaji wa Kimokouwa Longido wakiangalia mifugo iliyokufa kwa ukame.

Watoto wa kimasai wa kijiji cha Kimokouwa wakilisha mbuzi katika miti mikavu Mfugaji akiswaga ndama walio salia baada ya Ng'ombe wake zaidi ya 700 kufa kwa ukame.
Rais Jakaya Kikwete juzi alitembelea Wilaya ya Longido kuangalia athari za Ukame na upungufu wa chakula uliopo Wilayani humo na kuahidi kuwapatia msaada.
Blogu hii ya jamii inawaomba viongozi wa serikali kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na bila usumbufu.
Posted by MROKI On Monday, August 24, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo