MSTARI WA NYUMA-Kushoto kwenda kulia:- Nadir Haroub 'Canavaro', Jerson, Tegete, Juma Dihile, Haruna Moshi na Said Swedi.
MBELE-Kushoto kwenmda kulia:- Nurdin Bakar, Geofrey Bony, Mrisho Ngasa, Juma Jabu, Shedrack Nsajigwa na Nizar Khalfan.
Kikosi cha Stars kitakachokuwa katika safari ya Ivory Coast ni makipa Shaaban Dihile (JKT Ruvu), Deogratius Munishi (Simba) na Farouk Ramadhani (Miembeni). Walinzi: Shadrack Nsajigwa, Nadir Haroub, Amiri Maftah (Yanga) Erasto Nyoni, (Azam FC), Salum Swed (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Juma Jabu (Simba). Viungo: Nurdin Bakari, Athumani Iddi, Gofrey Bonny, Abdi Kassim (Yanga) Henry Joseph, Haruna Moshi (Simba), Nizar Khalfani (Moro United) na Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar). Washambuliaji: Mussa Hassan Mgosi (Simba), Jerry Tegete, Mrisho Ngassa, Kigi Makasy (Yanga), Uhuru Selemeni (Mtibwa Sugar).
Wachezaji wapya waliotangazwa na Maximo katika timu hiyo mapema mwezi huu, ambao ni Mwinyi Kazimoto wa JKT Ruvu na Zahoro Pazi wa Mtibwa Sugar wameachwa katika kikosi kiendacho Ivory Coast.
Kwa mujibu wa habari za ndani ya kambi ya Stars zilizopatikana leo jioni, wachezaji wengine ambao hawatakuwemo katika kikosi hicho ni kiungo Jabir Aziz wa Simba ya Dar es Salaam na Salvatory Ntebe wa Azam.
WAKATI HUOHUO wachezaji hoa wanaotaraji kuondoka keshokutwa nchini wamelalamikia kutokupatiwa posho zao kwa muda sasa na kufanya hali zao kuwa ngumu na familia zao. habari zaidi http://www.habarileo.co.tz/michezoburudani/?id=15943






0 comments:
Post a Comment