Nafasi Ya Matangazo

February 17, 2009

Mwanamuziki wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma, Joseph Maina, amekufa ghafla Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti tando hili, kiongozi wa Msondo Ngoma, Muhidin Gurumo alisema Maina alifikwa na mauti leo asubuhi akiwa ndani ya daladala, akienda kazini.

Alisema Maina alikuwa akielekea studio alikokuwa akutane na wenzake kwa ajili ya kurekodi albamu mpya ya bendi hiyo, ambayo tayari baadhi ya nyimbo zimeshakamilika.

“Alikuwa kwenye daladala kutoka Temeke Mikoroshini kwenda kazini Mwenge, ndipo mauti yalipomfika na hivi sasa mwili wake uko Temeke hospitali ,” alisema Gurumo. Enzi za uhai wa Peter Maina (kushoto) akiwa na Marehemu Moshi Wiiliam (katikati) na Mzee Mzima Gurumo. Picha hii ilipigwa nami tare 2/4/2003 katika ukumbi wa Diamond Jubilee katika mpambanao wa Msondo na DDC Mlimani Park.
Posted by MROKI On Tuesday, February 17, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo