Nafasi Ya Matangazo

November 19, 2008

Wakazi wa Dar es Salaam wakipita karibu na vyuma vya uzio uliowekwa katika eneo la Manzese Darajani ambao uliwekwa kuzuia watu kukatiza hovyo barabara ya Morogoro eneo hilo, ili watumie daraja lakini uzio huo umeanza kuanguka na mamlaka husika hazijachukua hatua ya kufanya ukarabati wa uzio huo tangu uanze kuangua takriban mwaka sasa. Je lengo la uzio huu umesha kamilika au ndo kila mmoja anasubiri mwenzake afanye?.
Mateja nao wanakodolea macho vyuma hivyo kuviuza kama screpa.
Posted by MROKI On Wednesday, November 19, 2008 2 comments

2 comments:

  1. Nchi imejaa ubabaishaji kuanzia juu mpaka chini,jiji lina mkuu wa mkoa,mkuu wa wilaya,meya,madiwani.viongozi kibao hakuna utekelezaji,bongo yetu hiyo kazi ipo.

    ReplyDelete
  2. Mie ndio nashangaa kila siku, tunakua wepesi kuchangamkia miradi fulani ili watu waibe. Wakishakamilisha wizi wao wanaangalia sehemu nyingine, sio ile waliojenga waiangalie na kuihudia vema. Ile methali ya "usipoziba ufa utajenga ukuta" inathibisha hapo. Maana baada ya kurekebisha sehemu ndogo ya uzio huo. Baadae itabidi vinunuliwe vyuma vipya baada ya wasmalia wema kuvisitiri kwa ma skrepa.

    Sio vibaya, maana wahusika hawaoni umuhimu wa uzio huo tena. Sijui kwa nini hatuwezi kutunza vitu?

    Halmashauri ya jiji na wahusika wengine hawaoni hivyo? Au ndio kwa sababu imetokea Mansese, hivyo hamna anayejali. Nafikiri ingekua imetokea Masaki au sehemu za mafisadi wangerekebisha haraka haraka.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo