Msemaji wa familia ya Mazula, Dk. Charles Lugora aliliambia HabariLeo jana msibani hapo kuwa Kapteni Mazula alifariki jana saa nne asubuhi baada ya kubanwa ghafla na ugonjwa unaodhaniwa kuwa ni pumu.
Kwa mujibu wa msemaji huyo utaratibu wa mazishi ya rubani huyo utafahamika leo baada ya kikao cha familia kilichotazamiwa kufanyika jana saa moja usiku nyumbani kwake namba SGX 4617 K.
Marehemu ameacha mjane mmoja na watoto wawili walioko Marekani wanaotarajiwa kuja wakati wowote kuanzia leo ambao ni (Brian na George). Mtoto mwingine wa Mazula alifariki kwa kupigwa risasi yeye na mpenzi wake miaka miwili iliyopita nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment