Kuanzia leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Mashimba.
The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;
BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?
MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?
BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?
MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa
BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?
MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali.Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.
BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?
MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa
BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?
MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa
Read more: UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA - BongoCelebrity
0 comments:
Post a Comment