Nafasi Ya Matangazo

August 07, 2016





Rais Dk John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakisali katika ibada ya Jumapili katika Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato mkoani Geita.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na na Padre wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato Henry Mulinganisa mara baada ya kuwasili kwenye kanisa hilo.
 Rais Dk John Pombe Magufuli akiimba wimbo wa Amani pamoja na Kwaya ya Kanisa la  African Inland Church la Chato Mkoani Geita mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo.


Shekhe wa Bakwata Wilaya ya Chato Hassan Issa Mnubi akiongoza dua ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli nje ya Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab Chato Mkoani Geita.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
 ***********
RAIS Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Agosti, 2016 ametembelea Msikiti na Makanisa yaliyopo Chato Mjini Mkoani Geita na kuendelea kuwasihi Watanzania kuombea amani na utulivu katika nchi bila kujali tofauti za dini, makabila na kanda wanazotoka.


Rais Magufuli ametoa ujumbe huo mara baada ya kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, na baadaye kutembelea Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Stephano Parokia ya Chato, Kanisa la African Inland Church la Chato na kumalizia katika Msikiti wa Omar Bin -L-Khattab wa Chato.

Dkt. Magufuli amesema pamoja na Watanzania wote kuungana kuombea amani na utulivu pia hawana budi kutekeleza kwa vitendo Maandiko Matakatifu ya Biblia yasemayo "Asiyefanya kazi na asile" kwa kuhakikisha kila mmoja anachapakazi kwa juhudi na maarifa ili kuharakisha maendeleo ya Taifa.

"Ndugu zangu nawashukuru sana, muendelee kuliombea taifa hili, taifa letu ni la umoja, sisi wote ni Watanzania, tuendelee kumuomba mola wetu, kudumisha amani yetu, kujenga umoja wetu kwa dini zote, makabila yote na vyama vyote, kwa sababu mola wetu anatupenda sisi sote" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, mara baada ya kuwasalimu waumini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Rais Magufuli ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo jipya la Kanisa hilo ambapo amefanikiwa kukusanya Shilingi Milioni moja za papo kwa papo.

Tayari Dkt. Magufuli alishachangia ujenzi huo kwa kutoa Shilingi Milioni kumi tarehe 03 Aprili, 2016 na ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo.

Katika Msikiti wa Omar Bin-L-Khattab na Makanisa ya Anglikana na African Inland Church Rais Magufuli amechangia Shilingi Milioni tano kwa kila moja kwa ajili kuendeleza na kukarabati majengo.
Posted by MROKI On Sunday, August 07, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo